×

Wasomaji wa Championi, Spoti Xtra Wazidi Kuliwania Gari

Wasomaji wa  Manzese-Bakhresa, Dar es Salaam, wakisoma gazeti la Championi.

WAKAZI wa Jiji la Dar, maeneo ya Manzese, Magomeni, Kigogo-Sambusa, Buguruni na vitongoji vyake Machi 13, 2020 walipitiwa na kikosi cha mauzo na usambazaji cha magazeti ya Championi ambacho kilikuwa kikiinadi Bahati Nasibu ya Baba Lao ambayo mshindi anatarajiwa kuondoka na gari jipya aina ya FunCargo.

 

Akiinadi Bahati Nasibu hiyo, Mkuu wa Idara ya Masoko ya Magazeti ya Global, Anthony Adam, aliwahamasisha wananchi hao kununua magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili kushiriki Bahati Nasibu hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Global, Anthony Adam (mwenye maiki),  akiwaelewesha wananchi waliokuwa katika Soko la Ilala jinsi ya kujishindia gari jipya aina ya FunCargo.

Akiwaelekeza jinsi ya kushiriki bahati nasibu hiyo, Anthony  aliwaambia:  “Unachotakiwa kufanya ni kununua magazeti hayo na kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili na kujaza jina lako, namba yako ya simu, anwani yako na umri wako.

Dogo Janja wa Kigogo-Sambusa, Dar,  akionyesha kuponi yake baada ya kununua gazeti la Championi na kushiriki Bahati Nasibu hiyo.
Wasomaji wa Manzese-Chama wakipata elimu ya kushiriki Bahati Nasibu ya Baba Lao kutoka kwa  Anthony Adam.

“Hapo utakuwa umemaliza kujaza kuponi hiyo na unachosubiria ni siku ya kuchezeshwa bahati nasibu hiyo”.

Sambamba na kujishindia gari, Anthony amesema kuna zawadi nyingine nyingi ambazo zitatolewa kila mwezi kuelekea kwenye droo hiyo ya kujishindia gari.

Alizitaja zawadi hizo kuwa ni pamoja na simu za mkononi za kisasa almaarufu kwa jina la Smart Kitochi na nyinginezo.

Anthony akiwaelekeza wafanyabiashara wa Soko la Buguruni jinsi ya kushiriki Bahati Nasibu hiyo.
Msomaji akinunua gazeti la Championi kutoka kwa Anthony ili kuijaza kuponi yake na kujiweka mkao wa kusubiri ndinga hiyo.

Na Richard Bukos

EXCLUSIVE :KAREN AFUNGUKA MAZITO MAGUMU ANAYOPITIA AMTAJA BABA YAKE

Leave a Comment