HATIMAYE ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa shauku kubwa na wanunuzi wa magazeti bora ya michezo Tanzania, Championi ambalo lipo mtaani kwa Sh 800 na Spoti Xtra ambalo ni Sh 500, itafanyika Machi 25 na washindi kibao watasepa na zawadi zao.
Shindano hili ambalo ni kubwa ambapo mshindi atajishindia gari, limepokelewa kwa kishindo na wanunuzi wa magazeti ya michezo ambao mbali ya kufurahia habari na makala bora wanajiongezea nafasi ya kushinda zawadi kibao.
Akizungumza kuhusu mpango uliopo kwa sasa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na lengo kubwa ni kurejesha shukrani kwa wasomaji wa magazeti yanayofanya vizuri sokoni.
“Tumeamua na tumedhamiria kuwa karibu na wasomaji kwa kuanza kwenye shindano letu kubwa la Jishindie Gari, droo ya kwanza natarajiwa kufanyika Machi 25 ambayo itakuwa siku ya Jumatano.
“Ni rahisi sana kumpata mshindi, na kushirki ni kununua gazeti lako la Championi au Spoti Xtra kwa kadiri uwezavyo, hakuna kikokomo kwani unavyoshiriki zaidi unajiongezea nafasi ya kushinda gari.
“Droo ya Kwanza itakuwa ni kwa ajili ya kutafuta washindi wa Smart Phone, T-Shirt na zawadi nyingine ndogondogo za papo kwa hapo, na kwa washiriki wanajio ngezea nafasi ya kushinda zawadi kubwa ya gari jipya kabisa,” alisema.


