×

Dereva Aliyembeba Mgonjwa, Wengine 27 Arusha Hawana Corona


WATU 27 waliofanyiwa uchunguzi kama wameambukizwa ugonjwa wa virusi vya Corona, akiwemo dereva wa teksi aliyembeba mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa huo nchini,  Isabella Mwampamba, wamebainika hawana virusi vya ugonjwa huo, Wizara ya Afya imesema.

 “Tumefuatilia watu 27 waliokuwa karibu na mgonjwa wa Corona Arusha akiwemo dereva, sampuli za wote zilichukuliwa na wote hawana virusi vya Corona.  Majibu yamechukua muda kwa sababu tulipima mara tatu kujiridhisha”  Dr. Janeth Mghamba amesema. 

Leave a Comment