×

WWF KUWEKEZA MSITU WA HIFADHI WA VIKINDU

Shirika la hifadhi ya mazingira duniani la WWF ofisi ya Tanzania limesema katika maadhimisho ya saa ya dunia ambayo binadamu ulimwenguni kote wanatakiwa kutumia dakika 60 kuzima taa katika kuiheshimu siku hiyo kila mwishoni mwa mwezi machi.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo, Meneja Mawasiliano wa WWF ofisi ya Tanzania, Joan Tanesa amesema watatumia maadhimisho hayo kusaidia kuuboresha misitu kadhaa ukiwemo ule wa Vikindu, mkoani Pwani ambao awali ulikuwa ukidaiwa kutumwia waharifu kujificha.

 

Joan amesema wameanza kuuboresha msitu huo kwa kuweka taa za sola, viti vya kupumzikia na vivutio vingine na kuufanya kuwa sehemu ya utalii na watu kwenda kupumzika.

 

Pamoja na msitu huo Joan ameutaja na msitu wa Kazimzumbwi na Pugu na kusema kuwa misitu hiyo ndiyo inayosaidia kutoa hewa safi kwa wakazi wa jiji la Dar.

 

Katika kuielimisha jamii ya Watanzania kulinda mazingira wamefanikiwa kuwabadili mawazo wakazi wa Kisiwa cha Mafia ambao karibu wote shughuli yao ni uvuvi na kuwaelimisha kufanya shughuli zingine za kutafuta kipato ili kulinda mazingira ya bahari na kuacha viumbe wa baharini waongezeke.

 

Joan amesema kwa kiasi kikubwa wakazi hao sasa hivi wameshaelimika na wamewasaidia kuanzisha vikundi vya Vicoba kwa ajili ya kupata mitaji ya kufanya shughuli nyingine ambazo haziathiri mazingira.

1.Joan akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

HABARI:NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL 

Leave a Comment