×

Sure Boy, Yanga ni Suala la Muda Tu

YANGA ipo katika hatua nzuri ya kukamilisha usajili wa kiungo wa Azam FC, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ anayewaniwa vikali na klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani na Twiga, Dar.

 

Sure Boy ni kati ya viungo wanaowaniwa vikali na klabu hiyo katika kuiboresha safu yao ya kiungo ambayo hivi sasa inachezwa na Haruna Niyonzima, Feisal Salum Fei Toto’, Issa Mohammed ‘Banka’ na Mapinduzi Balama ‘Kipenseli’.

 

Yanga imeingia vita ya kuwania saini ya kiungo huyo baada ya ripoti ya kocha Mbelgiji Luc Eyamel kuhitaji kiungo mwenye uwezo wa kukaa na mpira, kupiga pasi za mwisho na kuchezesha timu.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mipango yote ya kukamilisha usajili wa kiungo huyo imekamilika baada ya kufi kia makubaliano mazuri, hivyo ni suala la muda pekee kwa nyota huyo kutua Yanga.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kiungo huyo mwenyewe ameonekana kuhitaji kutua Yanga kwa kile kilichoeleza hivi sasa hana furaha na timu hiyo kutokana na kukosa namba ya kudumu katika kikosi hicho.

 

“Sure Boy hivi sasa hana nafasi ya kudumu ya kucheza katika kikosi cha kwanza tofauti na misimu mingine, hivyo anafi kiria kuachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu mara baada ya mkataba wake kumalizika.

 

“Kingine anavutiwa na bonasi ambazo wanapata timu hiyo chini ya wadhamini wao GSM ambayo inaelezwa hivi sasa hawapati Azam tofauti na misimu iliyopita.

 

“Kama unakumbuka vizuri hiyo ndiyo ilisababisha wachezaji Bocco (John), Nyoni (Erasto), Kapombe (Shomari) na Gadiel (Michael) waondoke kwenye timu hiyo,” alisema mtoa taarifa huyo. Alipotafutwa Ofi sa Habari wa Yanga, Hassani Bumbuli kuzungumzia hilo, alisema: “Usajili bado haujafunguliwa rasmi, hivyo hayo yote yanayoendelea ni tetesi, tusubirie muda ukifi kia tutaweka wazi.

 

Leave a Comment