×

Kesi ya Pili ya Kifo cha Ebola Yaripotiwa DRC

JAMHURI ya Kidemokrasia ya Congo imeripoti kesi ya pili ya kifo cha Ebola katika kipindi cha siku tatu baada ya nchi hiyo kupitia muda wa zaidi ya majuma sita bila ya kuripotiwa kesi mpya ya maambuzo ya ugonjwa huo.

 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza habari hiyo na kueleza kwamba, aliyeaga dunia kwa Ebola ni binti wa miezi 11 ambaye anasadikiwa kuambukizwa na mgonjwa aliyefariki kwa maradhi hayo juzi (Ijumaa) huko katika mji wa Beni.

 

Leo nchi hiyo inatarajiwa kutangaza rasmi kumalizika kwa ugonjwa huo katika nchi hiyo ambao umeua zaidi ya watu 2, 200.

 

Leave a Comment