×

Wagonjwa Watatu wa Corona Waongezeka TZ, Wafikia 49

WAZIRI wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid, ametangaza ongezeko la watu watatu wenye maambukizi ya virusi vya corona visiwani humo, hivyo kufanya idadi ya waathirika kufikia 12 kutoka 9 wa awali. Ongezeko hilo linafanya idadi ya waathirika nchini Tanzania kufikia 49.

 

“Wagonjwa wetu wawili waliokuwa wakipatiwa matibabu katika kituo cha Kidimi wameshapona #Covid19 na wameruhusiwa kurudi nyumbani, huku wakitakiwa kuendelea kubaki ndani bila ya kuchanganyika na watu wengine.” amesema waziri huyo.

 

Leave a Comment