×

Ishu ya Chama na Yanga… Simba Yakimbilia Kushtaki TFF

UONGOZI wa klabu ya Simba umefunguka kuwa unatarajia kupeleka barua kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuishitaki Yanga kwa kuvunja kanuni za usajili. Simba wamefi kia maamuzi hayo mara baada ya Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kufunguka kuwa wamefanya mazungumzo na kiungo wa Simba, Clatous Chama juu ya kutaka kumsajili mchezaji huyo.

 

 

Chama anayetajwa kuwa na thamani ya dola 350,000, inatajwa kuwa amebakiza mkataba wa miezi sita kwa mujibu wa Yanga, ambapo kwa upande wa Simba wao wanadai mchezaji huyo mkataba wake unamalizika mwaka 2021.

 

Akizungumzia ishu hiyo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Haji Manara amesema wanaipeleka Yanga TFF kwenda kujibu tuhuma za kiongozi wao Mwakalebala alizodai kuwa amefanya mazungumzo na Chama, ambaye bado ana mkataba na klabu hiyo, huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kanuni za usajili.

“Tunaipeleka Yanga TFF, kwenda kujibu tuhuma za Mwakalebela alizodai kuwa ameongea na Chama moja kwa moja kuhusu suala la kumsajili, wakati mchezaji huyo bado ana mkataba na Simba huku akijua kuwa ni kinyume cha sheria na utaratibu.

 

“Kwa hiyo wataenda kutolea ufafanuzi na safari hii watapata hasara zaidi ya ile waliyopata wakati wanamsajili Hassan Kessy, zile milioni 50 walizotoa ni ndogo, lazima ifi ke mahali Yanga inatakiwa wajifunze kupitia makosa yao wenyewe.

 

“Hiki kitu angekuwa amekizungumza mtu kama Antonio Nugaz au mtu mwingine, tungekaa kimya, ila kwa sababu ameongea makamu mwenyekiti, maana yake ni kitu ‘serious’, Chama bado ana mkataba mrefu na Simba,” alisema Manara.

 

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji Tanzania (Sputanza), Musa Kisoki, alisema: “Manara anachosema yupo sahihi, kama kweli Yanga wamefanya hivyo ni kosa kisheria na wana haki ya kupata adhabu kwa mujibu wa sheria. Mwakalebela alinukuliwa kuwa amefanya mazungumzo na Chama, juu ya kutaka kumsajili na mazungumzo yao yanakwenda vizuri, ambapo meneja wa mchezaji huyo aliiambia Yanga, mteja wake amebakiza miezi sita katika mkataba wake.

Leave a Comment