×

Kiba Afunguka Cheed na Killy Kutimka

IKIWA ni siku moja tangu wasanii wake wawili killy na Cheed waondoke kwenye lebo yake ya Kings Music Records, msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa Kings Music ni kama chuo na kwamba alikuwa akiishi na vijana hao kama ndugu zake.

 

“Tumefundishana mengi, naona sasa wamejiona wamehitimu, wakaamua kuondoka, tuwatakie kila la kheri. Vijana hao walinifuata usiku wa juzi wakamueleza juu ya uamuzi wao na mimi nikawapa baraka zangu zote za mwisho na baadaye alfajiri wakaposti uamuzi wao.

 

Aidha, Alikiba ameongeza kuwa nyimbo na kazi zote walizowahi kufanya wakiwa katika lebo yake ni mali yao na hawezi kuzizuia kwani “ni vijana wazuri” amesema Kiba.

Leave a Comment