×

JPM: Dawa Zilizopulizwa Dar ni Upuuzi, Hakuna Lockdown DSM – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amezungumza na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona. Matangazo ya kikao hicho yatarushwa mubashara kutoka Chato Mkoani Geita leo Aprili 22, 2020.

 

Nawashukuru kwa kuja kunipa ‘briefing’ za jinsi tunavyoendelea kupambana. Nimekubaliana na hatua mnazoendelea kuzichukua katika kipindi hiki. Napenda kushukuru Watanzania ambao kwa nyakati za maombi tulizotangaza kwa siku 3, wote walishiriki.

 

“Nawapongeza madaktari, manesi na wahudumu wa afya wanaoendelea kutoa huduma kwa waathirika kwani wameonesha moyo wa uzalendo. Naomba Watanzania tuendelee kuchukua tahadhari. Ugonjwa huu upo. Tahadhari ni muhimu sana. Napenda niwashukuru Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kuhakikisha usalama wa Taifa letu unakuwepo usiku na mchana.

 

“Lakini pia taarifa zetu ziendane na ukweli hasa katika watu wanaopona. Nina taarifa kwamba mpaka leo tulikuwa na wagonjwa 284, lakini naambiwa karibu 100 ya wagonjwa walishapona. Hizi takwimu za wagonjwa wanaopona nazo zitangazwe ili kuwaondolea hofu wananchi.
“Hakuna virusi wanaokufa kwa ‘fumigation’, kilichofanyika Dar es Salaam cha kupuliza dawa yenye kemikali (fumigation) ni upuuzi. Wanaokufa kwenye fumigation ni mende na si virusi ikiwemo virusi vya Corona.
“Nawashauri Watanzania mtengeneze barakoa hapa hapa nchini kwa usalama wetu, isijekutokea tukaletewa barakoa kisha tukaambukizwa, tuwe makini hata na misaada ya vifaa hivi tunavyopewa vya kujikinga.
“Endeleani na moyo huo wa uzalendo, mnafanya kazi ya Mungu ya kuwahudumia Watanzania, msivunjike moyo. Serikali ninayoiongoza ipo pamoja nanyi. Ninatambua kazi kubwa mnayoifanya.
“Kuna hili la kwamba kila anayekufa sasa ni corona, kwani malaria na magonjwa mengine yameacha kuua? Naomba Watanzania muwapuuze wanaopotosha kwenye mitandao, IGP hao wako shughulika nao na TCRA pia, sio kila anayekufa ni corona, tusipeane hofu.
“Benki ya Dunia wametoa ofa ya nchi zilizoambukizwa corona kukopa, naomba nchi za Afrika tusimame kuwaomba wakubwa hawa watusamehe madeni badala ya kutaka tuendelee kukopa huku wanataka riba, watusamehe hata kwa asilimia, ili hili fedha tukapambane na corona.
“Nawapongeza viongozi wa Dini na Watanzania kwa ujumla kwa kuitikia wito wa kuliombea Taifa kwa siku tatu dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. Ninaamini Mungu wetu ni wa huruma atatusikiliza na siku moja tutalishinda hili gonjwa.
“Navipongeza vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuilinda Nchi yetu hasa katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya COVID-19. Nimekubaliana na hatua mnazoendelea kuzichukua katika kipindi hiki.
“Wapo wanaotoa mawazo ya kuifunga Dar, haiwezekani kamwe, Dar ni kitovu ambako asilimia kubwa ya mapato inapatikana, hatuwezi tu kuifunga kisa corona, Dar ina watu million 6, hatuwezi kuwafungia, kesho tena Mwanza tuifunge hapana, hatuwezi kufanya lockdown Dar.
“Tutangaze pia na wanaopona sio wanaokufa tu, inawapa watu hofu kwamba ukipata corona lazima ufe, kwani maralia haiui? Nimegundua baadhi ya wanaopotosha kwenye mitandao wengine si Watanzania, namba zao ziko kwenye nchi za jirani wanawachafua tu Watanzani.
“Usipewe kitu cha mtu yeyote usiyemuamini, kikawa chanzo cha kusababisha Corona kwa wananchi very innocent,Magufuli.

Leave a Comment