×

APR Wafungukia Usajili Wa Kagere

INAELEZWA kuwa uongozi wa APR FC ya Rwanda upo katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu ujao.

 

Taarifa za ndani kutoka APR, zinadai kuwa rais wa klabu hiyo Jack Musemakweli amefanya mawasiliano na wakala wa Kagere, Patrick Gakumba akiulizia uwezekano wa kupata saini ya mchezaji huyo.

 

Kagere ambaye kwa sasa bado yupo Rwanda kwenye mapumziko ya janga hili la Corona, mkataba wake na Simba umebakiza mwaka mmoja kufikia tamati.

Championi Ijumaa lilimtafuta Msemaji wa Klabu ya APR, Clever Kazungu ili kujua ukweli wa taarifa hizo ambapo alisema: “Sina taarifa za kuwa rais wa klabu yetu amewasiliana na wakala wa Kagere, kwa sababu taarifa hizo zinaweza kuwa ni za ndani sana ambazo kwangu bado hazijanifikia.

 

“Lakini pia kwa upande wangu naweza nikasema siyo rahisi kwa Kagere kuweza kuja kucheza APR kwa sasa, kwa sababu levo aliyo nayo siyo ya kurudi kuja kucheza Rwanda, inatakiwa aende mbele zaidi ya hapa, lakini kubwa zaidi bado ana mkataba na Simba wa muda mrefu.”

Leave a Comment