×

Walioambukizwa Corona Kenya Wafikia 320

 

WIZARA ya Afya nchini Kenya imesema idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona sasa imefika 320 baada ya leo kutangaza visa vipya 17  vilivyotokana na sampuli 668 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.  Kati ya hao, 12 ni kutoka miji ya Mombasa na watano Nairobi.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya nchini humo, Dkt. Mercy Mwangangi, amesema wagonjwa 15 walichukuliwa na maafisa wa afya baada ya kuambatana na wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa awali huku wawili wakiwa ndani ya karantini.

 

Wakati huo huo, Kenya pia imethibitisha kwamba wagonjwa sita wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha idadi ya waliopona nchini humo kufikia 89.

Leave a Comment