DAR: WAKATI nchi ikiwa kwenye janga kubwa la mlipuko wa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19, kwa mastaa wa muziki, Hamisi Baba ‘H.Baba’ na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni tofauti, kwani wako kwenye bifu zito kisa magari, RISASI linakupa habari kamili.
Bifu hilo linakuja baada ya Diamond kuonyesha gari lake jipya aina ya Rolls Royce katika mtandao wake wa Tik Tok ambapo H.Baba naye baada ya kuliona, akaposti kwenye ukurasa wake wa Instagram gari aina hiyohiyo na kuandika maneno yaliyoonesha anampiga dongo staa huyo.
H.Baba aliandika maneno haya yaliyosomeka hivi; “Hahahhahahahahahaha no fakefake no rangi ya nyumba chezea Og wewe.”
Maneno hayo yaliamsha hisia za mashabiki wake kwenye mtandao huo wakidai kuwa, ameandika maneno hayo kumkejeli Diamond kwamba kanunua gari fake na siyo orijino.
Haikuishia hapo, Diamond naye alijibu mashambulizi kwa kurekodi kwa video magari matatu yakiwa barabarani huku akisema; “Raha ya magari haya uwe nayo ya kwako, siyo ukodi, bado zile mbili.”
Wambea wa kwenye mtandao huo wa kijamii walikata majibizano ya wawili hao na kusambaza vilivyo huku wakidai wawili hao walikuwa wakirushiana vijembe vya magari.
Baada ya kuona habari hizo, Risasi Jumamosi lilimvutia waya H.Baba ambaye ndiye alianza kumchokoza Mondi au Diamond na kuulizwa ambapo alijibu kwa dharau kuwa hamjui msanii huyo.
“Simjui Diamond, kwani unayemuongelea ni msanii wa nini,” alisema H.Baba na kukata simu, hata alipotafutwa tena hakupokea, simu yake iliita tu mpaka ikakatika yenyewe.
STORI: MEMORISE RICHARD, RISASI
