×

Wakili Gaudiosus Ishengoma Afariki Dunia


WAKILI msomi wa FB Attorneys, Gaudiosus Ishengoma,  amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne, Aprili 28, 2020, katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

 

Enzi za uhai wake,  Ishengoma alikuwa mwana-Yanga kindakindaki na ni miongoni mwa mawakili maarufu nchini ambapo baadhi ya mawakili wenzake wamekuwa wakimuelezea kuwa ni mzuri katika kesi za jinai.

 

Kabla ya kuwa wakili wa kujitegemea waiwahi kuwa wakili wa serikali kwa miaka minane kabla ya kujitegemea.

Leave a Comment