
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Ibrahim Peter (26) ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma akisomea Shahada ya Sayansi ya Biolojia.
Anatuhumiwa kuandika na kusambaza ujumbe wa kupotosha jamii kuhusiana na Dawa ya #COVID19 katika makundi ya WhatsApp kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Miongoni mwa jumbe alizosambaza ni kwamba ‘Dawa ya #COVID19 inatakiwa utwange pilipili kichaa sufuria moja halafu changanya na maji vikombe 5 na kunywa kutwa mara saba kwa muda wa siku tatu na siku ya nne chuma upupu kisha jipake mwili mzima.’
Kamanda wa Polisi Mkoani humo, ACP Simon Maigwa amesema mtuhumiwa amekamatwa katika Kijiji cha Mnyele Wilaya ya Nyasa na kitendo alichofanya ni upotoshaji, taratibu zinakamilishwa ili aweze kufikishwa Mahakamani.