MKUUwa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amegawa bure sukari kiasi cha kilo 5,000 iliyokamatwa katika mpaka wa Namanga unaotenganisha Tanzania na Kenya ikiingizwa nchini kwa njia ya magendo.
Aliigawa sukari hiyo jana Jumanne, Aprili 28, 2020, kwa watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo mayatima na wazee baada ya kuipokea kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyokuwa imeikamata.
