×

Burundi Yaanza Rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu

KAMPENI za uchaguzi wa urais utakaofanyika Mei 20, 2020,  zimeanza leo ambapo mgombea kupitia chama tawala (CNND-FDD), Evariste Ndayishimiye na Agathon Rwasa wa Chama cha Upinzani (CNL) wamezindua kampeni zao.

 

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (CEN), Pierre Claver Kazihise, amewaonya vikali wale wote watakaokwenda kinyume na sheria, huku Waziri wa Afya akiwakumbusha wananchi kuzingatia kanuni za kuepuka #COVID19.

 

Mgombea wa chama tawala tayari amepata uungwaji mkono kutoka vyama vya FNL, Muungano wa COPA na wafuasi wa UPRONA wanaounga mkono kundi la Isidore Mbayahaga.

 

Waziri wa Usalama, Alain Guillaume Bunyone,  amewataka wagombea kujiepusha na kauli za uchokozi zinazoweza kuhatarisha usalama katika kipindi hiki cha kampeni zitakazomalizika Mei 17.

 

Leave a Comment