×

Mahakama Yaamuru Zitto Akamatwe

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana Jumatano, Aprili 29, 2020, iliamuru kukamatwa kwa kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kwa kukiuka masharti ya dhamana katika kesi yake ya uchochezi inayomkabili.

 

Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shaidi, ametoa agizo hilo baada ya kiongozi huyo kushindwa kufika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa kwa shauri lake.

 

Hakimu huyo amesema kuwa hata wadhamini wa mshtakiwa huyo (Zitto) hawakufika mahakamani hapo kueleza yanayomsibu mshtakiwa.

 

Mahakama imepanga Mei 29, 2020, kutoa hukumu ya kesi hiyo ya uchochezi ambapo Zitto anatuhumiwa kulihusisha Jeshi la Polisi katika mauaji ya watu zaidi ya 100 mkoani Kigoma.

Leave a Comment