×

Wakili Msando Ashikiliwa Polisi – Video

KAIMU Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Koka Moita, amesema wakili wa kujitegemea, Albert Msando,  ameitwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano.

 

Alipoulizwa kama kushikiliwa kwake kunahusisha yale aliyoongea juzi wakati akikabidhi vifaa ya kujikinga na #COVID19, alijibu kuwa hana taarifa kamili na suala hilo halijakaa sawa kulizungumzia.

 

Aidha, amethibitisha kuwa Msando ameitwa Polisi kwa mdomo kama ambavyo alitumia yeye (Msando) kuzungumza, na kuwa hakuna nguvu iliyotumika.

 

Moita amesema, “Kama ambavyo alitumia mdomo kuzungumza, na kuja polisi pia imetumika kauli ya kumuita.” Amesema pia mahojiano yakikamilika atatoa taarifa.


Juzi wakati akigawa vifaa hivyo Msando alisema; “Ni kweli na niseme bila kuficha hali ni mbaya, kwa Arusha hali ni mbaya. Ndugu waandishi lazima mfike mahali muweke mguu chini mseme ukweli ili wananchi, serikali na kila anayehusika atambue tupo katika hali mbaya ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuchukua hatua.”

 

Aliongeza, “Mkirudi nyuma na kuogopa kusema, tutazikana. Hii ndiyo nafasi yenu, tusipozungumza, msipoandika na kusema ngoja tutoke nje tukatafute ukweli na tuuseme kama ulivyo, basi huu ugonjwa hautaondoka kirahisi.”

Leave a Comment