×

Siri Ya Niyonzima Kuoa Mke Wa Pili Yafi Chuka

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, juzi Jumanne aliishika mitandao baada ya kusambaa picha na taarifa kuwa amefunga ndoa, huku siri ya kiungo huyo kufunga ndoa hiyo ikiwekwa wazi.

 

Taarifa zinasema kuwa, Niyonzima alifunga ndoa hiyo ambayo ni ya pili na mwanamke Mtanzania, Cassandra Rayan, huko Bagamoyo mkoani Pwani.

Ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema kuwa Niyonzima ameamua kuoa mke wa pili kwa sababu hapendi kuwasumbua watoto wake, ambapo mara nyingi amekuwa akiwahamisha pale inapotokea amerudi Rwanda au kuja Tanzania.

 

“Tunaamini sasa Haruna atatuliza akili yake, kwa sababu mara nyingi alikuwa anaiwaza sana familia yake hasa watoto, mara nyingi alikuwa anawahamishahamisha shule, kwa hiyo hivi sasa atakuwa na amani kwa sababu kama watoto wakiwa Dar watakuwa na mama mdogo, wakiwa Rwanda watakuwa na mama yao mkubwa,” alisema Bumbuli.

STORI NA ISSA LIPONDA | SPOTI XTRA

Leave a Comment