×

Video: Rais Magufuli “Fenesi, Mbuzi Nao Wana Corona”

Rais Dk John Magufuli haamini usahihi wa majibu ya vipimo katika Maabara Kuu ya Serikali kuhusu ugonjwa wa corona.

Ameagiza ufanyike uchunguzi na kama kuna vitendo vya jinai wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

 

“Mimi ni mwanasayansi, ninajua ninachokizungumza…Watanzania bado tupo kwenye elementary stage (hatua za mwanzo), tusipanic”amesema Rais Magufuli.

 

Ameyasema Chato mkoani Geita baada ya kumuapisha Dk Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Kwa mujibu wa Rais, huenda kuna walioambiwa wana virusi vya corona wakati si kweli na huenda baadhi yao wamepoteza maisha kwa sababu ya hofu.

 

“Kuna mchezo wa ajabu unafanyika kwenye vipimo hivi…kwa hiyo lazima kuna kitu fulani kinafanyika” amesema na kuongeza kuwa huenda wahusika wanatumiwa na mabeberu.

 

Amesema, katika siku zilizopita maabara hiyo ilikuwa ikitoa matokeo mengi positive kuhusu maambukizi ya corona na amesema jambo hilo linatia mashaka.

 

Ameagiza ufanywe uchunguzi kufahamu vifaa hivyo vikoje na vinafanye kazi kwa kuwa si kila kifaa ni kizuri na huenda kuna watumishi kwenye maabara hiyo wanatumika wafanye hujuma kwa kuwa hali ya sasa ni vita.

 

Ametoa mfano kuwa kuna oil ya gari ilipekwa kupimwa kwa jina la Jabir Hamza (30) majibu yakawa negative, fenesi kwa jina la Sarah Samwel (45) majibu hayakuwa wazi, na Papai kwa jina la Elizabeth Anneh (46) majibu yalikuwa positive.

 

Amesema, kilipelekwa kipimo cha ndege kwale majibu yakawa positive, mbuzi yakawa positive, na kondoo yakawa negative.

 

Dk Magufuli amesema, kuna maswali mengi ya kujiuliza kuhusu vipimo hivyo na huenda kuna kitu fulani Watanzania au wanasayansi hawajakielewa.

Leave a Comment