×

Rais Magufuli Agawa Pikipiki 12 kwa Maofisa Tarafa

 

RAIS John Magufuli ametoa pikipiki 12 kwa maafisa tarafa mkoani Rukwa ili ziweze kuwasaidia kutekeleza majukumu yao ya kiserikali katika kata wanazozihudumia.

 

Pikipiki hizo zimetolewa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Aprili 6. 2019, baada ya kufanya kikao-kazi na maafisa tarafa wote nchini alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, amemshukuru rais kwa kutimiza ahadi hiyo huku akiwasisitiza maafisa hao kutumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kusimamia mapato, miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao  na kusikiliza kero za wananchi.

 

Akitoa  shukurani kwa niaba ya maafisa tarafa wenzake, Afisa Tarafa wa Kasanga, Andrew Ngindo, baada ya kumshukuru rais alimuomba mkuu wa mkoa kuona kutafuta uwezekano wa kutengewa bajeti ya mafuta pamoja na matengezo kwa pikipiki hizo ili ziendelee kuwarahisishia utekelezaji wa majukumu yao.

 

Leave a Comment