SAA chache baada ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kuwafuta uanachama wabunge wake wanne, Anthony Komu (Moshi Vijijini), Joseph Selasini (Rombo), David Silinde (Momba) na Willfred Lwakatare (Bukoba Mjini) kutokana na kukiuka miongozo ya chama hicho, Lwakatare amezungumza na Global TV akiwa Bungeni jijini Dodoma na kutoa tamko lake kuhusu uamuzi huo wa chama chake.
