Mamia ya wananchi huko mjini Tabora wamejumuika katika mazishi ya aliyekuwa Afisa mrakibu msaidizi wa Jeshi la Polisi ASP MASOUD MOHAMMED ambaye amezikwa kwenye makaburi ya familia yake huko katika kijiji cha Manoleo manispaa ya Tabora.
ASP Masoud ambaye kwa siku za hivi karibuni Afisa huyo wa jeshi la Polisi amekuwa maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii kwa namna ambavyo amekuwa akionekana anasoma kitabu kitukufu cha Quraan,alikutwa umauti akiwa chumbani kwake mnamo Mei nane mwaka huu huko Ukerewe mahali ambako alihamishiwa kikazi akiwa ni mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.
