SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amesema hakuna mwenye mamlaka ya kumfukuza mbunge yeyote isipokuwa yeye ambaye aliwaapisha.
“Wabunge mnaapishwa na Spika na karibu wote nimewaapisha mimi hapa, sasa wabunge wangu niliowaapisha yaani msiwe na wasiwasi, hakuna cha nini wala nini. Vikao vya majungu hivyo havifanyi kazi, eti mtu mmoja katika nchi hii anajifanya yeye ana mamlaka ya kufukuza wabunge anavyotaka hii haiwezekani, mliofukuzwa endeleeni kuhudhuria Bungeni tutawalinda,” amesema.
Kauli hii inakuja saa chache baada yaChadema kuwafuta uanachama wabunge wake wanne ambao ni Wilfred Lwakatare, Joseph Selasini, David Silinde na Anthony Komu kwa madai ya kukiuka taratibu za chama na kukikashifu chama hicho.
