×

Ijumaa Sexiest Girl 2019/20… Poshy Queen, Mimi Mars Ni Mshikemshike

Posh Queen.

BAADA ya kubaki warembo wawili, Posh Queen na Mimi Mars, sasa ni mshikemshike nguo kuchanika ambapo kumekuwa na upigaji kura usiopishana kiasi cha kushindwa kutoa uamuzi wa nani ajitwalie taji hili.

 

Katika shindano hili, warembo 20 walipitishwa na mashabiki wao na wamekuwa wakipigiwa kura za kutoka katika kumtafuta Mrembo Mwenye Mvuto wa Gazeti la IJUMAA (Ijumaa Sexiest Girl 2019/20) ambapo kwa sasa ushindani umekuwa mkubwa mno baina ya warembo hawa wawili.

Mimi Mars.

Mratibu wa shindano hili ambaye ni Mhariri wa Gazeti la IJUMAA, Sifael Paul amesema baada ya kubaki warembo watatu, ushindani umekuwa ni mkali mno.

“Sasa kazi ipo kwa Poshy Queen (13) na Mimi Mars (14).

“Unachotakiwa kufanya ni kupiga kura ya nani atoke kwa kuandika jina au namba yake ya ushiriki kisha unatuma kwenda WhatsApp namba; 0713 750 910,” alisema Sifael na kuongeza; “Wadhamini wanakaribishwa kudhamini kinyang’aro hiki kwa kuwasiliana na namba hiyo hapo juu.


Leave a Comment