×

Sun Kika Ft. Angel Benard “My Hiding Place” – (Official Video)

 

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Sun Kika ameachia video mpya ya wimbo wake uitwao “My Hiding Place” (Maficho Yangu) ambao amemshirikisha mwimbaji mahiri wa Gospel nchini, Angel Bernard.

 

Video ya wimbo huu imefanyika nchini Marekani.

 

Sun Kika anasema;

“My Hiding place” ni ushahidi wa maisha yangu.
Nilizaliwa nikiwa liwazo kwa wazazi wangu waliopoteza watoto wengi kabla yangu. Nimepoteza kaka na dada wengi waliokufa kati ya mwaka mmoja hadi minane. Nimemwona Mungu akipigana vita vyangu, akiniokoa na kifo mara nyingi.  AMEKUWA MAFICHO YANGU.

 

Unaposikiliza wimbo huu ninaomba Mungu akulinde na awe maficho yako wakati huu ambapo ulimwengu umejaa woga wa virusi vya corona.  Tunamtumikia Mungu mwenye uwezo, anaweza kufanya mengi tunayoweza kumwomba na kufikiria.

Mungu akubariki.
Sun Kika.

 

Leave a Comment