×

Ndemla Asaini Miaka Miwili Simba

RASMI kiungo mkabaji wa Simba, Said Ndemla ameongezewa mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kukipiga kwenye klabu hiyo kwenye msimu ujao baada ya kufikia muafaka mzuri na mabosi wake.

 

Ndemla ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu akiwa na wenzake Shiza Kichuya, Hassani Dilunga, Pascal Serge Wawa, Yusuph Mlipili na Sharaff Eldin Shiboub.

 

Awali, kiungo huyo alikuwa anatajwa kutimkia Yanga ambayo ilikuwa inatajwa kuwania saini yake kwa ajili ya kuiimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kiungo huyo amesaini mkataba huo tangu wiki mbili zilizopita baada ya kiungo na viongozi wa timu hiyo kufikia muafaka mzuri.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kiungo huyo amebakishwa Musa Mateja,Dar es SalaamSimba kutokana na nidhamu kubwa aliyoionyesha akiwa na timu hiyo licha ya kutokuwepo katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kinachonolewa na Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.

 

Aliongeza kuwa kingine kilichombakisha ni uwepo wa viungo wakabaji wachache katika timu hiyo, licha ya kuwepo mipango ya kushusha kiungo mwingine mkabaji wa kimataifa mwenye uwezo mkubwa zaidi yake.

 

“Viongozi wamekubaliana kuwabakisha wachezaji wao waliowalea tangu wakiwa wadogo U20 kwa lengo la kutoondoka ndani ya kikosi hicho kutokana na uvumilivu waliokuwa nao wa kutoihama timu hiyo ambao ni Ndemla na Mkude (Jonas).

 

“Hivyo viongozi wamekubaliana kumbakisha, lakini amebakishwa kwa makubaliano ya kupambana katika timu ili apate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

 

“Ndemla amekubaliana na hayo yote waliyokubaliana nayo huku akiomba mkataba wake uwe wa wazi utakaomruhusu kuondoka muda wowote kama akipata timu nje ya nchi,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa hivi karibuni aliwahi kuliambia Championi kuwa: “Kama uongozi tumepanga kuwabakisha wachezaji wote ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu kwa gharama yoyote lengo ni kuhakikisha tunasuka kikosi imara kitakachofanya vizuri katika msimu ujao.”

Stori na Musa Mateja,Dar es Salaam

BANDARI ya TANGA KUBORESHWA, DC SHIGELA Atoa MAELEZO ya MRADI

Leave a Comment