×

Arusha: Madereva 21 wa Kenya Wakutwa na Corona Namanga

 

MKUUwa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema kufuatia ongezeko la visa vya #COVID19 mipakani, mkoa huo umeanzisha utaratibu wa kuwapima madereva wa malori wanaotokea Kenya kupitia Namanga.

 

Sampuli zilichukuliwa tarehe 14,16 na 18  mwezi Mei ambapo madereva 44 walipimwa Mei 14 na iligundulika 14 wana maambukizi ya #CoronaVirus na 30 wapo salama. Kati ya madereva hao 14, 11 ni raia wa Kenya, 1 ni kutoka Uganda na uraia wa madereva wengine wawili unahifadhiwa.

 

Majibu ya sampuli 23 za Mei 16 yalithibitisha madereva 10 wote Wakenya wana #COVID19 na wengine 13 walikutwa hawana. Sampuli za Mei 18 bado zinaendelea kufanyiwa vipimo na majibu yatatolewa yakishapatikana.

 

Leave a Comment