×

Young Aibuka Na Muonekano Mpya

WINGA wa zamani wa Manchester United, Ashley Young, juzi alionekana akiwa na muonekano wa tofauti baada ya kuacha nywele.

 

Winga huyo ambaye kwa sasa anaichezea Inter Milan alionekana akiwa tofauti na hali aliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu akiwa na Man United kwa kuwa kila mara alionekana akiwa na upara.

Baadhi ya komenti kwenye mitandao ambayo picha hiyo imewekwa zimesema kuwa staa huyo amebaki hivyo kwa kuwa ameshindwa kwenda saluni akiogopa kuambukizwa virusi vya Corona.

 

Juzi Inter Milan walianza mazoezi yao na Young al-ionekana kuwa tofauti na jinsi alivy-okuwaga awali.

 

Winga huyo am-baye pia anaweza kucheza beki wa pembeni alijiunga na timu hiyo kwenye usajili wa Januari na ame-shaanza kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

Leave a Comment