×

Mshauri wa Waziri Mkuu Matatani kwa Kupuuza ‘Lockdown’

Boris Johnson (picha ya jana) ambaye polisi wanachunguza tukio lake la kupuuza sheria za ‘lockdown’ za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

MSHAURI mkuu wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Dominic Cummings, ameingia matatani kwa kuondoka jijini London na kwenda kuwaona wazazi wake huko County Durham, wakati nchi hiyo iko chini ya amri ya watu kutotembea ovyo (lockdown) wakati akiwa pia na dalili za kuambukizwa virusi vya corona.

 

Cummings na mke wake wanadai walikwenda huko ili kujitenga wenyewe, alisema msaidizi wake, Laura Kuenssberg, akiongeza kwamba, hata hivyo, wawili hao kila mtu alikaa katika nyumba yake.

 

Jambo hilo limeleta tafrani kutoka chama cha upinzani ambacho kinataka maelezo ya jambo hilo na hatua za haraka zichukuliwe dhidi yake Cummings, ikiwa ni pamoja na kumwachisha kazi kwa kukiuka maagizo ya serikali yake.

Dominic Cummings akiwa na Waziri Mkuu Boris Johnson (picha ya Septemba mwaka jana) anayetakiwa kumfukuza kazi mshauri wake huyo.

Waingereza wametaka hatua dhidi yake zichukuliwe wakisema hapawezi kuwepo sheria moja kwao na nyingine kwa  Dominic Cummings.

Dominic Cummings (kulia) akiwa na mkewe Mary Wakefield.

Habari za karibuni zinasema polisi tayari wamemhoji Cummings kuhusu tukio hilo.

 

Safari ya kutoka London kwenda Durham kwa wazazi wa Cummings.

Leave a Comment