×

Mke wa Waziri Mkuu Asaka Dhamana ya Kumuuguza Mumewe

MKE  wa Thomas Thabane, aliyekuwa waziri mkuu wa Lesotho, Maesaiah Thabane, anayeshtakiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mke wa mumewe, Lipolelo Thabane, anatafuta kuachiwa huru kwa dhamana ili kumhudumia mumewe ‘anayeugua’.

Maesaiah alishtakiwa mnamo Februari kwa mauaji hayo siku mbili kabla ya kutawazwa kwa mumewe mwaka 2017.

Alizuiliwa  gerezani kabla ya mahakama kuu nchini humo kumuachia huru katika hali isiyoeleweka kwa dhamana ya dola 57.    Siku ya Ijumaa, mahakama ya rufaa ilifutilia mbali dhamana yake na akarejeshwa kizuizini siku ya Jumatano baada ya kusafiri kutoka taifa jirani la Afrika Kusini ambapo mumewe anapata huduma za matibabu.

Nyaraka mpya za ombi la dhamana zilizoonekana siku ya Alhamisi, zimesema kuwa Thabane amegunduliwa kuwa na saratani na hali ya kupoteza fahamu na huenda akafariki iwapo mkewe hatakuwa karibu yake.

Ombi hilo pia linakanusha kuwa Maesaiah alihusika na jukumu lolote katika mauaji ya Lipolelo.

Leave a Comment