
MSANII mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini, Johari Chagula ”Johari”, amefunguka kuwa wasanii wa sasa hivi hawafanyi kazi kwa weledi bali wanafanya kazi kwa kukurupuka.
Akizungumza na Amani Johari amesema kuwa katikasanaa ya zamani wasanii walikuwa lazima waingie kwenye mafunzo ya kuigiza lakini ni kwa sasa imekuwa tofauti yaani kila mtu amekuwa msanii.
“Kwenye mambo ya uigizaji kuna mambo mengi sana yamebadilika kwa sababu sanaa ya zamani ilikuwa ni sanaa ya mapokezi, kwa hiyo kile tulichokuwa tukikifanya watu wanakipokea kwa mashamsham kwa sababu kilikuwa na mafuzo ndani yake lakini sanaa ya sasa imebadilika kwa sababu hadi watazamaji nao wanajiona ni wajuaji. Pia kuna wasanii ambao wanababaisha kwenye suala zima la uigizaji, watu wanakurupuka tu na kwenda kushuti wakati sisi tulikuwa tunaingizwa kwenye mafunzo mpaka ujue nd’o uigize,” alisema.
Stori: Khadija Bakari