NAHODHA Msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amet-amba kuwa kikosi chao kipo kamili kutetea ubingwa wao na sasa wamepanga kurudi na moto mkali zaidi kuliko ilivy-okuwa hapo awali.
Akizungumzia programu za mazoezi zinazoendelea katika Uwanja wa Simba Mo Arena uli-opo Bunju jijini Dar, Zimbwe Jr alisema:
“Tunaendelea vizuri na mazoezi ya kujiandaa na michezo yetu iliyosalia, licha ya kwamba tulikuwa nyumbani kwa muda mrefu lakini kila mmoja alikuwa akifuatilia ratiba ya mazoezi bin-afsi tulizoachiwa na kocha Sven.
“Najua swali kubwa kwa wengi ni kutaka kuona tunarudi namna gani na kama tumeathiri-ka na janga hili la Corona, lakini nipende kuwahakikishia kuwa tutarudi tukiwa bora zaidi ya tulivyokuwa hapo mwanzo ili kutetea ubingwa wetu kwa mara nyingine tena.”
Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa imejikusanyia pointi 71 katika michezo yao 28 iliyocheza mpaka sasa na inahitaji pointi 15 tu katika mechi kumi zilizobaki ili kutangaza ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo.
Stori: JOEL THOMASDar es Salaam