
WAANDAMANAJI wanaopinga ubaguzi wa rangi wameliondoa sanamu la Mfalme Leopold II lililokuwa mjini Antwerp ambalo limekuwa likilalamikiwa na wanaharakati kwa muda mrefu.

Mfalme Leopold II anajulikana kwa kuwa na utawala wa chuma kwa makoloni ya Afrika ambapo katika utawala wake aliwaua takriban raia wa Congo milioni 10.
Alitawala kuanzia mwaka 1885 hadi mwaka 1908, na tafiti zimeonesha kuwa alikuwa anakosolewa kwa ukatili aliokuwa akiufanya tangu kipindi hicho.

Maandamano ya wanaopinga ubaguzi wa rangi yamefanya pia majina ya baadhi ya mitaa kuangaliwa namna ya kuyabadilisha kama yanaashiria ubaguzi au ukatili ambao uliwahi kufanywa na wenye majina hayo.