
MKALI wa Hip Hop Bongo, Bonventure Kabongo ‘Stamina’ amesema suala la kumuoma msamaha aliyekuwa mkewe ni jambo la siri na la watu wawili.
Stamina amesema haliwezi kuwa jambo la kuweka hadharani kwani wakati wanakubaliana kuwa kwenye uhusiano hakuwaambia watu.
“Mimi sijaweka uhusiano wangu wala kumuonesha mke wangu, ule ni muziki tu, halafu sijui kwa nini Watanzania hawaamini kwamba naweza nikamuimbia mtu mwingine. Nimeongelea ndoa, sijamuongelea mwanamke wangu.
“Masuala ya kuombana msamaha ni mambo binafsi ya watu wawili, kama yeye ameomba msamaha au mimi nimeomba msamaha ni vitu binafsi na hata ikitokea hivyo lazima ianze kwa watu wawili siwezi kuja kuvisema hadharani kwa watu,” amesema Stamina.