
MSANII kunako tasnia ya uche-keshaji hapa nchini, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ amesema kuwa wasanii wa nje wanafanya muvi zao kisomi ndiyo maana wanauza kuliko wasanii wa Bongo.
Kingwendu amesema, kitu ambacho kinafanya soko la filamu Bongo lishuke ni kutokana na watu kufanya kazi kwa kukurupuka na ukosefu wa vifaa ambavyo vina uwezo wa kutosha.
“Kiukweli wenzetu wa nje ya nchi, wanaweza sana; kwanza wanafanya kazi zao kisomi, yaani ukiangalia filamu za Ki-Nigeria, hautamani kuondoka, wenzetu kule wanaweza wakafanya filamu kwa mwaka mzima, lakini uje sasa Bongo, filamu wiki tu ishatoka ipo sokoni na pia wale wanavyo vifaa vya gharama na ndiyo maana wenzetu wanatupiga bao hata kwenye masoko,” alisema Kingwendu.