
RAIS John Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) asubuhi leo Jumatano ya Juni, 17, 2020, amechukua fomu ya kuwania kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu.
Amekabidhiwa fomu hiyo na katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, kwenye makao makuu ya chama hicho mkoani Dodoma.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, amesema anaanza mapema mchakato wa kutafuta wadhamini ili awahi kurejesha fomu hiyo mapema.
Mwenyekiti huyo wa CCM amesema amekuwa akipigiwa simu na makada wa chama hicho, ambao wamemwahidi kumdhamini.
“Naomba nianze zoezi hili la kutafuta wadhamini, nitaenda mikoa yote kwa sababu nimekuwa nikipigiwa simu wakisema wanataka kunidhamini hivyo nitarejesha fomu yangu kwa wakati,” amesema.