×

Chameleone, Daniella wagonga miaka 12 ya ndoa

KATIKA ujumbe wake kwa mkewe, Daniella mapema wiki hii, mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa Afrika Mashariki, Jose Chameleone amemshukuru mno mama huyo wa watoto wake kwa kumvumilia kwenye ndoa hadi sasa wamegonga miaka 12.

 

“Heri ya miaka 12 ya ndoa yetu Mama Abba. Kumbukumbu ni nyingi sana kichwani mwangu, nashukuru Mungu kukupata wewe na kwa pamoja tumetengeneza familia ya kupendeza,” ameandika ujumbe huo Chameleone kwenda kwa Daniella.

 

Ndoa hiyo ilifungwa mwaka 2008 katika Kanisa la Mtakatifu James Bbiina lililopo Mutungo nchini humo.

Kama zilivyo ndoa nyingi za mastaa, wawili hao nao wamepita kwenye milima na mabonde kiasi cha kudaiwa kutaka kuachana, lakini walifanikiwa kusimama tena.

 

Wawili hao wamejaaliwa watoto watano ambao ni Abba, Amma, Alba, Alfa na Xara Amani Mayanja.

 

IJUMAA | STORI: KAMPALA, UGANDA

Leave a Comment