×

Arteta Amhofia Guardiola

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema anaona hatari kuvaana na bosi wake wa zamani, Pep Guardiola.

 

Arteta atakutana na Guardiola katika mchezo wa Premier utakaochezwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Etihad.

 

Kocha huyo alikuwa msaidizi wa Gaurdiola katika Klabu ya Manchester City kabla ya kupewa mkataba na Arsenal.

 

“Itakuwa ni hatari, kwa hilo siwezi kukataa hata kidogo hasa kukutana na Guardiola.

“Pale namfahamu kila mmoja kwa kuwa nimekuwa pale kwa miaka minne.

 

“Nina hamu ya kupambana nao, tulichokuwa tunakisubiri sasa naona kinakaribia kurejea, tulitamani kurudi uwanjani kupambana na kufanya kile tunachokipenda.

 

“Kuvaana na Man City kwangu ni kitu spesho na zaidi ninaangalia mbele kuona timu yangu inafanya vizuri,” alisema.

LONDON, England

Leave a Comment