×

Misingi No Itaamua Nani Agombee Siyo Lazima Mbowe – Video

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema ndani ya chama hichio, hakuna kanuni inayomzuia mwanachama kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote katika chama, cha msingi ni kuandika barua kwenda kwa katibu mkuu wa chama kama walivyofanya akina Tundu Lissu na wagombea wengine ambao ametimiza kanuni hizo ndani ya chama kuwania urais.

 

Hayo yamesemwa leo, Alhamisi, Juni 18, 2020, na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene, wakati akifanya mahojiano maalum na Kipindi cha Front Page kinachoruka kupitia +255 Global Radio.

 

“Mchakato wa ndani ya chama tangu umetangazwa kumekuwa na majadiliano mengi sana, na sisi tunaruhusu mijadala. Mwaka 2015 mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe naye alitangaza nia ya kugombea, hata mwaka huu misingi ndiyo itakayoamua nani agombee siyo lazima awe mwenyekiti.

 

“Kama wanajiamini wamefanya kazi kubwa, walipaswa kwenda kuthibitisha kwenye uchaguzi badala ya kuogopa ushindani. Wagombea wetu walinyimwa fomu, kuenguliwa kinyume na taratibu. Tulishajipanga kuwapa ushindani mkubwa sana lakini wakavuruga uchaguzi, na sisi tukaubatilisha.

 

“Kama wanajiamini wamefanya kazi kubwa, walipaswa kwenda kuthibitisha kwenye uchaguzi badala ya kuogopa ushindani. Wagombea wetu walinyimwa fomu, kuenguliwa kinyume na taratibu. Tulishajipanga kuwapa ushindani mkubwa sana lakini wakavuruga uchaguzi, na sisi tukaubatilisha.

 

“Chadema ndiyo chama pekee ambacho mpaka sasa kina sera, tuliizindua mwaka 2018 ikifafanua malengo 12 ya chama. CCM hata mkiwapigia simu sasa hivi, hawana sera ambayo wameshaitangaza.

 

“Wanasema eti kwa nini hakupelekwa hospitali za serikali baada ya tukio. Huduma ya kwanza haimlazimishi mtu kwenda hospitali gani, cha msingi inakuwa ni kuokoa maisha na kuhakikisha upo sehemu salama. Ndicho kilichofanyika.

 

“Kumekuwa na makandokando mengi sana kuhusu suala la mwenyekiti wetu Freeman Mbowe kushambuliwa. Msaidizi wa nyumbani wa Joyce Nkya anashikiliwa mpaka sasa kinyume na kanuni, analazimishwa kusema kitu ambacho ni tofauti na kilichotokea.

 

“Dhana kuwa kwenye chama kuna unyanyasaji wa kingono ni tuhuma nzito, lakini tuhuma hizo zinatolewa wakati gani ndio swali kubwa. Mtu mwenye akili timamu atajiuliza kwanini tuhuma ziibuke wakati wametolewa kwenye chama.

 

Leave a Comment