
STAA wa muziki wa Bongo Fleva na memba wa lebo ya Wasafi Classic Baby ( WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny, amefunguka sababu ya kufuta posti zote katika ukurasa wake wa Instagram.
Rayvanny amesema kuwa, muda mwingi amekuwa akitumia katika kuweka mambo yake sawa na si kuwa bize na mitandao ya kijamii.
“Kwa sasa siko sana mitandaoni, kuna mipango naweka sawa. Ni maisha tu, kuna muda unatakiwa kutuliza akili, mashabiki zangu wajue niko sawa, nawaandalia vitu vizuri kwa ajili ya muziki wangu, na niko sawa na Wasafi,’’ alisema Rayvanny ambaye kwa sasa kuna tetesi kuwa yuko mbioni kujitoa katika lebo hiyo.
STORI: HAPPYNESS MASUNGA, AMANI