The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Exclusive Nandy Azungumzia Ngoma Yake Na Harmonize

0
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Faustina Mfinanga (Nandy) amefanya Exclusive Intervie Kupitia kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia Global Radio Juni 18, 2020 ameeleza namna ambavyo amejipanga kuendelea kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva ambapo amesema kuwa njia moja wapo itakayomfanya vizuri ni kujituma ili mashabiki zake waweze vitu bora.
Katika mahojiano yake kupitia kipindi hicho msanii huyo mambo ambayo amefunguka yalikuwa hivi;
“Muda sahihi ukifika tutaingia tu kwenye hizo tuzo za BET na tuzo kubwa duniani, tujifunze kupitia hao walioingia, itafika wakati tutaingia hata watano cha msingi tuendelee kufanya ngoma zilizo bora”
“Mimi Billnass huwa tunataniana sana licha ya kuwa ni wapenzi kwa hiyo kitu changu kizuri yeye anaweza kunitania, kwenye video ile ya mimi na Harmonize alikuwepo kama ‘director ame-play part’ kubwa sana hivyo hakumaindi chochote,”.
“Tumetoka kwenye kikao juzi na menejimenti, tuna ngoma zetu na kuna uchaguzi na kuna kazi nyingi hivyo Mungu akijalia mwakani tutafunga ndoa,”
“Kwenye maisha yangu mimi kwa kweli sijawahi kudanga, ubaya kwamba wasichana wanaodanga ukiwapa ushauri wanaweza kukuvamia, cha kuwashauri ukimwi upo hivyo nawaomba  tutumie kinga,”
“Siyo rahisi, dunia nzima ushaona wapi watu wanafanya sherehe kwa ajili ya msanii fulani, kikubwa tunampongeza Diamond kwa kufikisha Views Bilioni 1 YouTube. Umoja siyo tu kufanya sherehe, tunampongeza Diamond kwa kutuwakilisha vyema,” alisema Nandy.

Leave A Reply