
RAIS John Magufuli leo Juni 22, 2020, Ikulu, Dar es Salaam, amemwapisha Idd Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha anayechukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo, baada ya kutenguliwa Juni 19, 2020.
Wakati huohuo hapohapo Ikulu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idi Kimanta, amemwapisha Kenan Kiongosi, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Baada ya hafla hiyo, Rais Magufuli aliwataka walioapishwa kwenda kufanya kazi kulingana na viapo vyao na kujiepusha na mambo binafsi ambayo huvuruga utendaji wa kazi za serikali.
Naye Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo, aliwataka viongozi hao wakachape kazi kutokana na imani aliyowapa rais kwa msingi wa kuwaamini ili waende kuyarekebisha yale yaliyowashinda watangulizi wao hususan mkoani Arusha.
Kwa habari zaidi, sikiliza video iliyoko chini: