
MKURUGENZI wa Global Publishers, Eric Shigongo amesema kuwa ukitaka kupata familia ya watoto wenye uelewa darasani, ipo haja ya kijana kutafuta mtu ambaye alikuwa na uelewa darasani na kisha kuanzisha familia.
Shigongo alisema, familia zote zenye watoto wenye uelewa darasani, ukifuatilia kwa makini utagundua wazazi watoto hao walikuwa na uwezo na uelewa mkubwa wakati wakiwa shuleni, hivyo vinasaba vya wazazi hao vilikuja kurithishwa hadi kwa watoto.

Akizungumza kwenye kipindi cha darasa kinachorushwa na +255Global Radio Jumatatu hadi ijumaa, Shigongo alisema hakuna muujiza wa kuweza kupata watoto waelewa darasani kama wazazi waliozaa watoto hao hawakuwa na uelewa darasani, hivyo njia pekee ya kuepuka suala hilo ni kijana kutafuta wenza ambao angalau wana uelewa fulani.
“Ukikutana na mtoto ambaye haelewi darasani, basi ukichunguza kwa makini, utagundua kuwa hata wazazi wake, walioana wakiwa wote wanatatizo la uelewa, hakuna muujiza wa kubadilisha familia yako isipokuwa kutafuta mwanamke au mwanaume ambaye alikuwa na akili shuleni,” alisema Shigongo.

Katika darasa hilo, Shigongo utoa somo akiwa pamoja na mwalimu Rodrick Nabe ambapo kwa upande wa Nabe alisema kuwa: “Kuanzia Jumatatu yan wiki ijayo, tutakuja kutoa somo nzuri la namna ya kupata wenza ambao ni waelewa.”
Sambamba na hilo somo kubwa ambalo lilimetolewa leo, ilikuwa ni juu ya wafanyabiashara kutakiwa kuijalui na kuithamini biashara yao pamoja na kuipa thamani bidhaa pamoja na wateja wake ili kuweza kujenga misingi imara ya biashara husika.
Huku wakikisitiza pia kuwa na moyo wa kutaka ushindani wa kibiashara dhidi ya wafanyabiashra ambao wanauza bidhaa zinazofanana.
Jishindie Simu Janja (Smart Phone) kwa kutazama kipindi bora cha *DARASA LA SHIGONGO* kupitia Global TV Online, kinachorushwa kila siku, Jumatatu-Ijumaa *Saa10:00 hadi Saa11:00 jioni*. Cha kufanya ni rahisi;
Ingia Youtube Channel ya Global TV kisha, *Subscribe*, na *Bonyeza alama ya kengele 🔔* (Notification bell). Kipindi kinapokuwa hewani, ingia kwenye LIVE CHART kisha *comment* na uandike namba yako ya simu. Watu 100 wa kwanza wataingia kwenye droo ya kujishindia Simu kila wiki.
DARASA LA SHIGONGO NDIYO MPANGO
MZIMA, MJULISHE NA MWEZIYO, *BONYEZA LINK HII KU SUBSCRIBE*:https://bit.ly/2AyVIvE
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx