×

Metacha Ampasua Kichwa Shikhalo

KIPA namba mbili kwa sasa wa Yanga raia wa Kenya, Farouk Shikhalo amekiri kuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uimara wa Metacha Mnata ambao amekuwa akiuonyesha kila mara.

 

Shikhalo amesema licha ya kuwa kocha Luc Eymael amemuamini zaidi Metacha, lakini yeye ataendelea kupambana na kufuata maelekezo anayopewa na walimu wake kwani anaamini wakati wake utafika na atapata nafasi ya kucheza.

Metacha Mnata

Shikhalo alitua Yanga wakati wa usajili wa dirisha kubwa akitokea Bandari ya Kenya na alikuwa chaguo la kwanza mbele ya Kocha Mwinyi Zahera, lakini baadaye mambo yakabadilika na tangu ligi iliporejea Juni 13, Metacha amecheza dakika zote katika mechi tatu akiwa na kiwango cha juu.

 

“Naheshimu maamuzi ya walimu kwa kumuanzisha Metacha lakini pia kwake ni changamoto ya kujiimarisha zaidi. Kila mchezo una falsafa yake na mwalimu anajua ni nani anastahili kuanza kwenye mechi husika, kukaa kwangu benchi haina maana kwamba siwezi, hapana, ni maamuzi ya mwalimu na kwa hali hiyo inanifanya nizidi kupambana ili kuwa bora.“Metacha anafanya kazi nzuri na kila mtu anaona lakini hilo haliwezi kunikatisha tamaa kwa sababu naamini uwezo wangu na itafika wakati nitaanza tena kucheza kama ilivyokuwa awali,” alisema Shikhalo.

STORI: Issa LipondaDar es Salaam

“MORRISON Atacheza DHIDI ya SIMBA, BADO ni MCHEZAJI wa YANGA” – KOCHA YANGA

Leave a Comment