The House of Favourite Newspapers

Kutendwa Kumewapa Maendeleo Shamsa, Faiza!

0
Shamsa Ford

STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amefarijiana na staa mwenziye ambaye ni mjasiriamali, Faiza Ally kuwa kutendwa na wanaume ambao wamezaa nao, kumewafanya wakawa na maendeleo.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Shamsa alisema yeye na Faiza wakizungumza wanasikilizana kwa sababu wamepitia machungu ya kulea wao watoto wenyewe tena kwa shida, lakini wamesimama.

“Mwanamke yeyote ambaye amepitia matatizo ya kulea mtoto mwenyewe, anaweza kujua nazungumza nini na ndivyo ilivyokuwa kwa mimi na Faiza, tunaweza kuzungumza lugha moja na pia ni watu tunaofarijiana sana kwa kweli na tunatoboa tu tukiwa wenyewe hivi hivi bila kuwa na wanaume pembeni,” alisema Shamsa ambaye anamlea mwanaye Terry.

 

Faiza yeye anamlea mwanaye peke yake aliyezaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

 

Stori:Imelda Mtema

Leave A Reply