PENZI la mwanamuziki kunako gemu la Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ na DJ Seven ambaye ni DJ wa mwanamuziki na C.E.O wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide, Rajab Abdul ‘Harmonize’, ni moto.
Video zilizosambaa za wawili hao wakiwa kwenye bethidei ya DJ Seven ziliwaonesha wakilishana keki kwa mahaba motomoto, huku Harmonize au Harmo akiwapongeza kwa tukio hilo.

Mambo yamekuwa moto kwani wawili hao kwani ni miongoni mwa kapo zinazozungumziwa zaidi baada ya juzikati kuposti picha wakiwa kwenye mavazi ya ndoa na kusemekana ndoa tayari, japokuwa hawakutaka kuweka wazi kuhusiana na ishu hiyo.
Linah amesema anaridhika na sapoti anayopata kuoka kwa DJ Seven, kwani amekuwa akimsapoti na kuonesha kumjali. Hii ni baada ya mwanamama huyo kuachana na mzazi mwenzake, Director Mchomvu ambaye amezaa naye mtoto mmoja