Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama pamba wakati alipokagua ghala baada ya kuzindua ununuzi wa zao hilo mkoani Katavi kwa msimu wa 2020/2021 kwenye Chama cha Msingi cha Ushirika cha Kasekese wilayani Tanganyika.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kuzindua ununuzi wa pamba Mkoani Katavi kwa msimu wa 2020/2021 kwenye Chama cha Msingi cha Ushirika cha Kasekese wilayani Tanganyika, Julai 4.gWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama pamba yenye kiwango cha daraja la kwanza iliyokuwa ikipimwa wakati alipozindua ununuzi wa zao hilo.