
DAVID Molinga ambaye ni mtupiaji namba moja ndani ya Klabu ya yanga, amesema kuwa wamekubaliana kwa pamoja kupata pointi tatu kwenye mchezo wao dhidi ya biashara United, kesho.
Molinga amefunga mabao 10 ndani ya Ligi Kuu Bara huku Yanga kwa ujumla ikiwa na mabao 38.
Yanga kesho itakaribishwa na Biashara United inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza ambaye alilazimisha sare ya bao 1-1 na Azam katika mchezo wao uliopita.

Molinga alisema: “Wachezaji tupo tayari na kila mmoja anajua kwamba tunahitaji pointi tatu, nafasi ambayo tupo kwa sasa ina ushindani mkubwa hivyo ili kuzidi kubaki kwenye nafasi tuliyopo ni lazima tushinde.
”Mpinzani mkubwa wa Yanga kwa sasa kwenye nafasi ya pili ni Azam FC mwenye pointi 59 baada ya kucheza mechi 32, tayari bingwa ni Simba.